9th June
2012
Dk. Hussein Mwinyi
Serikali imewatahadharisha na kuwakemea
wahudumu wa afya wote wenye tabia ya kuuza damu kwa wagonjwa kuwa hatua
kali dhidi yao zitachukuliwa.
Aidha hospitali zote zimeagizwa kuweka mabango yanayoonyesha kuwa damu
haiuzwi, na wananchi wametakiwa kutoa taarifa kwa viongozi pindi
wanapoona wahudumu wanauza damu.
Tadhari hiyo ilitolewa jana na Waziri Dk. Hussein Mwinyi wa Wizara ya
Afya na Ustawi wa Jamii wakati akitoa tamko la wizara hiyo kuhusu
maadhimisho ya siku ya wachangia damu salama duniani ambayo huadhimishwa
kila Juni 14 ambapo kitaifa hafla hiyo itafanyika mjini Moshi mkoani
Arusha.
"...wizara yangu inakemea na kulaani kitendo cha kuuza damu kwa wagonjwa
wakati inapatikana bure kwenye kanda zetu..." alisema na kueleza kuwa
kauli mbiu ya mwaka huu ni 'kila mchangia damu ni shujaa'.
Dk. Mwinyi alisema kuwa tangu kuanza kwa mpango wa damu salama nchini
2004, kumekuwa na mafanikio mbalimbali yakiwemo ya ongezeko la vituo vya
kanda kutoka vinne mwaka 2006 hadi vinane mwaka 2007.
Mafanikio mengine ameyataja kuwa ni ongezeko la ukusanyaji wa damu
kutoka chupa 52,000 mwaka 2005 hadi 140,000 mwaka jana ambapo mahitaji
halisi kwa mwaka ni wastani wa kati ya chupa 350,000 na 400,000 ingawa
malengo yaliyopo katika kipindi cha mwaka huu na mwaka ujao ni kati ya
chupa 180,000 na 200,000.
Alisema mafanikio mengine ni kupungua kwa kiwango cha virusi vya Ukimwi
kwenye damu inayokusanywa na vituo vya damu salama kutoka asilimia saba
mwaka 2005 hadi asilimia moja mwaka jana na uanzishwaji wa mfumo mpya wa
teknolojia ya habari na mawasiliano unaosimamia shughuli zote za
upatikanaji wa damu salama.
Hata hivyo, alisema kumekuwepo na changamoto nyingi zikiwemo za mahitaji
makubwa ya damu kuliko upatikanaji wake, uelewa mdogo wa jamii kuhusu
suala la uchangiaji wa damu kwa hiari, uuzwaji damu usio halali,
matumizi yasiyo sahihi ya damu katika hospitali na miundombinu hafifu
hasa ya barabara.
Dk. Mwinyi aliziomba taasisi mbalimbali na viongozi wa serikali, siasa,
dini na jamii kushirikiana na serikali katika jitihada hizi ili kunusuru
maisha ya wahitaji wa damu.
Kuhusu maambukizi ya Ukimwi, alisema takwimu zinaonyesha kuwa asilimia
kati ya tano na 10 ya maambukizi hayo husababishwa na mgonjwa kuongezewa
damu yenye virusi vya ugonjwa huo ingawa yapo magonjwa mengine kama
vile virusi vya homa ya ini na kaswende.
Maadhimisho hayo ambayo kidunia yanaadhimishwa mjini Seoul, Jamhuri ya
Korea, madhumuni yake hasa ni kuwashukuru na kuwashawishi wachangiaji
damu kujiheshimu ili waendelee kufanya hivyo, kuwatia moyo wasiochangia
kufanya hivyo na kuwahimiza wafanyakazi wa huduma za damu kuwatambua
wachangiaji.
Wakuu wapya wa wilaya hawana ofisi
SERIKALI imepoteza zaidi ya Sh5.4 bilioni kutokana na kulipa
mishahara kwa wafanyakazi hewa 9,949 katika kipindi cha miezi mitano
iliyopita.Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa alisema vitendo hivyo
vimekwamisha utekelezaji wa miradi mingine ya maendeleo ambayo
ingegharamiwa kwa fedha hizo.
Kauli ya Dk Mgimwa imekuja ikiwa ni
zaidi ya mwaka mmoja tangu Rais Jakaya Kikwete alipotoa agizo la
kudhibiti wafanyakazi hewa katika wizara na idara za Serikali.
Machi
mwaka jana, Rais Kikwete aliamuru kufanyika kwa ukaguzi katika idara
zote za serikali kutokana na kuwapo kwa taarifa kwamba kiasi cha Sh9
bilioni kilikuwa kimelipwa kama mishahara kwa wafanyakazi hewa katika
wizara tatu tu za Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Katiba na Sheria na Afya
na Ustawi wa Jamii.Rais alisema wahusika wa vitendo hivyo
walipaswa kubainishwa ikiwa ni hatua ya kukomesha mara moja wizi wa
fedha za umma kupitia mishahara hewa na kwamba Serikali haipaswi
kuwaruhusu watu ambao wameiibia Serikali fedha kuendelea kufanya kazi za
umma.
Lakini jana akifungua Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya
Fedha lililofanyika Dar es Salaam, Dk Ngimwa alikiri kuwapo kwa tatizo
hilo, mwaka mmoja tangu kutolewa kwa agizo hilo la Rais Kikwete.
Kutokana
na hali hiyo, alisema Serikali imechukua hatua za kukabiliana na
ufisadi huo kwa kuweka utaratibu wa orodha ya wafanyakazi kupitiwa kila
mwezi.Aliwataka wafanyakazi wenye tabia hiyo kuiacha mara moja akisema
Serikali iko makini na itawachukulia hatua kali wahusika wote.
Alisema
wiki ijayo itasomwa Bajeti ya Serikali 2012/13 ambayo imezingatia Dira
ya Taifa ya Maendeleo 2025 na imelenga ukuaji wa uchumi wa kiwango cha
kati, hivyo suala la udhibiti wa mapato ya Serikali halitakuwa na
mjadala.
“Tunataka kuleta hali bora ya maisha ya wananchi. Lengo
la Serikali ni kila mmoja kupata wastani wa pato la Dola za Marekani
3,000 (Sh3.8 milioni) kila mwezi ifikapo mwaka 2025,” alisema.
Alisema
bila udhibiti wa tatizo la mishahara ya wafanyakazi hewa, ni vigumu
kufikia lengo hilo hivyo kuwataka wafanyakazi wa wizara hiyo kujipanga
vizuri ili lengo hilo lifikiwe.
Alisema wafanyakazi wa Hazina
ndiyo wanaobeba jukumu hilo wakati Serikali inajitahidi kupambana na
mtikisiko wa kiuchumi hususan kipindi hiki cha kuelekea bajeti.Alisema
Serikali imeomba nguvu ya kujiongezea uwezo kutoka mashirika ya
kimataifa, nchi za Mashariki ya Kati na Asia.
Awali, Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi,
Ramadhan Khijjah alisema kuna tatizo la wafanyakazi wa wizara hiyo
kuogopa kuzungumza katika vikao vya baraza hilo.
“Watu waoga
huogopa kuzungumza. Wanawahofia wakuu wao wa idara jambo ambalo
halijengi,” alisema.
Alisema hali hiyo inachangiwa na walio wengi
kuogopa kuchukiwa na mabosi wao jambo ambalo alilipinga na kuwatoa hofu
akiwataka wawe wazi.
Alisema mabaraza hayo ndiyo sehemu ya
kukosoa, kuelekeza na kubainisha kasoro zilizopo ili hatua zichukuliwe
na kujenga mshikamano kwa manufaa ya Taifa na jamii kwa ujumla.
DK. Mwakyembe: Nishaonja kifo siogopi kufa
Waziri wa Uchukuzi, Dk.Harrison Mwakyembe, ameapa kuwa hataogopa vitisho
vyovyote kuwafukuza kazi watumishi wa mashirika, taasisi na idara za
serikali zilizopo chini ya wizara yake wanaokwenda kinyume cha utendaji
kazi kwani kama ni suala la kufa alishaonja kufa kipindi alipougua.
Alisema hayo juzi wakati akizungumza na wafanyakazi wa Chuo cha Bahari
kilichopo jijini Dar es Salaam baada ya kukitembelea ikiwa ni siku moja
baada kutembelea Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA).
“Nawahakikishia bandari itanyooka, nitapigana hadi dakika ya mwisho,
sitaogopa kufa maana kama ni suala la kufa tayari nilishaonja kufa
nilipougua sana,”alisema Dk.Mwakyembe.
Alisema nchi hii haisongi mbele kimaendeleo kutokana na maneno kuwa
mengi na kwamba katika ziara yake aliyoifanya katika Mamlaka ya Bandari
Tanzania (TPA) amekuta kuna uozo mwingi na kuahidi kusafisha wale wote
ambao wanatuhumiwa kuhusika na kashifa mbalimbali bandarini hapo.
Dk.Mwakyembe alisema wakati anachukua hatua za kusafisha kwa kuwang’oa
watumishi wabadhirifu katika taasisi, idara, mashirika yaliyopo chini ya
Wizara ya Uchukuzi, wanafunzi waliomaliza darasa la saba, kidato cha
nne na sita wakae mkao wa kula kwa ajili ya kuziba nafasi hizo.
“Na katika hili sitanii, hapa nitaomba kabisa wale wanafunzi waliomaliza
darasa la saba, kidato cha nne, sita na chuo kikuu waanze
kujioorodhesha kabisa majina yao maana nitawafukuza kazi watu wengi sana
katika wizara hii,” alisema Dk.Mwakyembe.
Aidha waziri huyo aliutaka uongozi wa Chuo cha Bahari kuwa wawazi kwa
wafanyakazi wao kwa kuwaeleza mapato na matumizi ili watumishi wasiwe
wanajenga hoja kwamba fedha zao zinaliwa.
Serikali yalipa Sh5 bilioni wafanyakazi hewa 10,000
SERIKALI imepoteza zaidi ya Sh5.4 bilioni kutokana na kulipa
mishahara kwa wafanyakazi hewa 9,949 katika kipindi cha miezi mitano
iliyopita.Waziri wa Fedha, Dk William Mgimwa alisema vitendo hivyo
vimekwamisha utekelezaji wa miradi mingine ya maendeleo ambayo
ingegharamiwa kwa fedha hizo.
Kauli ya Dk Mgimwa imekuja ikiwa ni
zaidi ya mwaka mmoja tangu Rais Jakaya Kikwete alipotoa agizo la
kudhibiti wafanyakazi hewa katika wizara na idara za Serikali.
Machi
mwaka jana, Rais Kikwete aliamuru kufanyika kwa ukaguzi katika idara
zote za serikali kutokana na kuwapo kwa taarifa kwamba kiasi cha Sh9
bilioni kilikuwa kimelipwa kama mishahara kwa wafanyakazi hewa katika
wizara tatu tu za Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Katiba na Sheria na Afya
na Ustawi wa Jamii.Rais alisema wahusika wa vitendo hivyo
walipaswa kubainishwa ikiwa ni hatua ya kukomesha mara moja wizi wa
fedha za umma kupitia mishahara hewa na kwamba Serikali haipaswi
kuwaruhusu watu ambao wameiibia Serikali fedha kuendelea kufanya kazi za
umma.
Lakini jana akifungua Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya
Fedha lililofanyika Dar es Salaam, Dk Ngimwa alikiri kuwapo kwa tatizo
hilo, mwaka mmoja tangu kutolewa kwa agizo hilo la Rais Kikwete.
Kutokana
na hali hiyo, alisema Serikali imechukua hatua za kukabiliana na
ufisadi huo kwa kuweka utaratibu wa orodha ya wafanyakazi kupitiwa kila
mwezi.Aliwataka wafanyakazi wenye tabia hiyo kuiacha mara moja akisema
Serikali iko makini na itawachukulia hatua kali wahusika wote.
Alisema
wiki ijayo itasomwa Bajeti ya Serikali 2012/13 ambayo imezingatia Dira
ya Taifa ya Maendeleo 2025 na imelenga ukuaji wa uchumi wa kiwango cha
kati, hivyo suala la udhibiti wa mapato ya Serikali halitakuwa na
mjadala.
“Tunataka kuleta hali bora ya maisha ya wananchi. Lengo
la Serikali ni kila mmoja kupata wastani wa pato la Dola za Marekani
3,000 (Sh3.8 milioni) kila mwezi ifikapo mwaka 2025,” alisema.
Alisema
bila udhibiti wa tatizo la mishahara ya wafanyakazi hewa, ni vigumu
kufikia lengo hilo hivyo kuwataka wafanyakazi wa wizara hiyo kujipanga
vizuri ili lengo hilo lifikiwe.
Alisema wafanyakazi wa Hazina
ndiyo wanaobeba jukumu hilo wakati Serikali inajitahidi kupambana na
mtikisiko wa kiuchumi hususan kipindi hiki cha kuelekea bajeti.Alisema
Serikali imeomba nguvu ya kujiongezea uwezo kutoka mashirika ya
kimataifa, nchi za Mashariki ya Kati na Asia.
Awali, Katibu Mkuu
wa Wizara hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi,
Ramadhan Khijjah alisema kuna tatizo la wafanyakazi wa wizara hiyo
kuogopa kuzungumza katika vikao vya baraza hilo.
“Watu waoga
huogopa kuzungumza. Wanawahofia wakuu wao wa idara jambo ambalo
halijengi,” alisema.
Alisema hali hiyo inachangiwa na walio wengi
kuogopa kuchukiwa na mabosi wao jambo ambalo alilipinga na kuwatoa hofu
akiwataka wawe wazi.
Alisema mabaraza hayo ndiyo sehemu ya
kukosoa, kuelekeza na kubainisha kasoro zilizopo ili hatua zichukuliwe
na kujenga mshikamano kwa manufaa ya Taifa na jamii kwa ujumla.
Wabunge wakataa bajeti ya Wizara
Makamo mwenyekiti(Hesabu za serikali za Mitaa)
idd Azzan
Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii wamegoma
kupitisha bajeti ya Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana kwa
kuwa imeshindwa kutoa mchanganua wa bajeti ya mwaka uliopita.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Jenista Muhagama, alisema hayo jana
wakati akizungumza na waandishi kuhusu suala hilo ambapo alisema kuwa
wameshindwa kuipitisha bajeti ya wizara hiyo kwa kuwa haijaonyesha kiasi
cha fedha ilichopewa na matumizi yake.
Alisema wizara hiyo ilitakiwa kutoa ufafanuzi sahihi kuhusu bajeti
iliyopita ili Kamati iweze kuipitisha lakini imeshindwa kufanya hivyo.
Muhagama alisema waliipatia muda wa kuonyesha ripoti ya mchanganua wa
bajeti iliyopita na kwamba matumizi ya miradi ya maendeleo hazikuwekwa,
hivyo Kamati haikuwa tayari kuipitisha bajeti hiyo.
Wakati huo huo, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati za Hesabu za Mashirika ya
Umma (POAC), Murtaza Magungu (CCM), ameitaka serikali kuipatia Bodi ya
Mazao Mchanganyiko na Nafaka kiasi cha Sh bilioni 10 kama mtaji ili
waweze kuingia katika ushindani wa biashara kwa lengo la kushusha
gharama za vyakula.
Alisema bodi hiyo itakuwa inafanya kazi yake ya kununua chakula kwa
wakulima na kuviuza kwa wananchi kwa gharama nafuu ili kushindana na
wafanyabiashara katika kushusha bei za vyakula.
Magungu alisema endapo serikali ikishindwa kuweka ushindani katika
biashara tatizo la mfumuko wa bei litaendelea kuwakabili wananchi.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za
Serikali za Mtaa ( LAAC), Idd Azzan, ameagiza Mkaguzi wa Ndani wa
Hesabu za Halimashauri ya Wilaya ya Nkasi kukatwa asilimia 15 ya
mshahara wake wa mwezi huu kutokana na uzembe aliouonyesha.
Alisema hakuna mchanganuo wa fedha dhidi ya miradi mbalimbali
iliyofanyika katika Halmashauri hiyo ambapo ilitakiwa ikaguliwe mahesabu
yake.
"Hatutaki kuona figure tunahitaji kuona huo mchanganuo wa matumizi ya
fedha yalivyofanyika ikifika Julai 8, muwe mmeshatupatia matumizi ya
miradi hiyo kwani mahesabu yenu yana mikanganyiko," alisema.
Alisema Mkaguzi wa ndani anatakiwa kulisimamia suala hilo kwa umakini na
kujua mchanganua ya fedha hizo za miradi zilivyotumika hivyo adhabu
hiyo itamfanya asimamie shughuli zake kwa umakini.